Januari 10, 2024 katika Dimba la Jamhuri Dodoma Majira ya Saa Kumi kamili za jioni, Timu yetu ya Wanawake inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania bara Fountain Gate Princess itacheza Mchezo wa ligi dhidi ya Yanga Princess, kuelekea mchezo huo basi unatakiwa kufahamu mambo haya.

NANI MBABE WA MWENZAKE?

katika Michezo Minne iliyopita ya Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania bara Fountain Gate Princess imefanikiwa kushinda mitatu huku Yanga Princess wakiambulia sare katika mchezo mmoja. Ni dhahiri Timu yetu ni wababe mbele ya Yanga Princess.

MAGOLI YA KUFUNGWA NA KUFUNGA.

Katika michezo hiyo minne iliyopita imeweza kuzalisha magoli Tisa. Fountain Gate Princess imefanikiwa kuifunga Yanga Princess magoli Sita huku Yanga Princess walifanikiwa kufunga magoli Matatu pekee. Hivyo ni dhahiri kwamba kwenye mchezo huo wa Dabi Fountain Gate Princess imekuwa bora sana kwenye kufunga mbele ya Yanga Princess.

WACHEZAJI WA KUCHUNGWA

Bila shaka Timu zote zimefanya usajili ili kuboresha vikosi vyao. Toka msimu umeanza tayari Kuna Nyota wameonyesha viwango vikubwa kiasi wanafanya kuwa Nyota wa kutizamwa kuelekea katika mchezo huo. Mchezaji wetu Amina Ramadhan tayari amefunga magoli matatu katika Michezo miwili ya Ligi Kuu huku Kwa upande wao Precious Christopher ambaye amefunga magoli matatu katika Michezo mitatu.

UTAKUWA MCHEZO WA AINA GANI?

Sio mchezo wa kwanza Kwa makocha wa pande zote mbili kukutana. Kocha wetu Juma Masoud wa amekutana mara Mbili na Kocha Haalubono Charles huku mchezo wa kwanza ukiisha Kwa sare ya 1-1 na kuamuliwa Kwa mikwaju ya penati katika fainali ya GETS International Tournament ambapo Timu yetu ilitwaa ubingwa Kwa mikwaju ya penati 12-11.

Lakini pia awamu nyingine ni katika katika mchezo wa kusaka mshindi wa Tatu wa Ngao ya Jamii kwa Wanawake na mchezo huo ulitamatika Kwa sare ya 0-0 na kuamuliwa pia Kwa mikwaju ya penati ambapo waliishinda Timu yetu. Hali hiyo inaonyesha makocha hao wamekuwa wakicheza Kwa Mbinu kubwa wanapokutana na huenda matokeo ya Michezo iliyopita walipokutana yanaweza kujirudia.

HALI YA KIKOSI

Kwa mujibu wa Taarifa kutoka Kwa Kocha Msaidizi wa Fountain Gate Princess Issah Shaban ameeleza kwamba hali Iko sawa ndani ya kikosi cha hicho hivyo Mashabiki wa Timu hiyo wanapaswa

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *