Mashindano ya Kashasha mwaka huu yatafanyika kuanzia mwezi Juni Tarehe 6 mpaka 11 ambayo yatafanyika katika Uwanja wa Fountain Gate uliopo katika Shule za Fountain Gate, Mlimwa C Dodoma.
Akizungumza katika Mkutano wa Waandishi wa Habari Country Meneja wa Fountain Gate Sports Academy Kelvin Shaaban amesema kwamba Mwaka huu yatahusisha Mataifa mbalimbali, hivyo kupewa jina la Kashasha Youth International Tournament.
Akiongeza juu ya Mataifa ya Jirani kushiriki mashindano hayo amesema kuwa tayari wameshatuma Mialiko. Lakini pia ameongeza kuwa ubora waliounyesha katika mashindano ya CECAFA na yale Afrika yaliyofanyika pale Durban Afrika Kusini imewavutia kushiriki
Lakini pia katika Mashindano hayo kutakuwa na semina ya Afya, Chakula na Sheria kwa wanamichezo, ili kuongeza uelewa kwa wanamichezo juu ya vitu vinavyowazunguka wao, hivyo waamuzi wataalikwa kufundisha sheria za Mpira wa miguu.
Katika kuhakikisha Watoto wanapata uhakika wa kuendeleza vipaji vyao Mawakala wamealikwa pia kuona vijana wakicheza ni nafasi Kwa vijana kupata fursa ya kufanikiwa kupitia Michezo.