Mara baada ya kuipa heshima Tanzania kwenye Mashindano ya Mpira wa Miguu yanayohusisha Shule za Sekondari barani Afrika Ukanda wa CECAFA, Timu ya Wasichana ya Sekondari Fountain Gate Dodoma imekabidhiwa Bendera rasmi kwenda kuiwakilisha Tanzania na Ukanda wa CECAFA katika ngazi ya Bara.

Bendera hiyo imekabidhiwa na Waziri wa Sanaa, Tamaduni na Michezo Mh. Balozi Dkt. Pindi Chana katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, huku akiwakumbusha kwenda kupambana kwa ajili Taifa.

Timu hiyo inatarajia kusafiri siku ya Tarehe 1 Mwezi Aprili Mwaka huu kuelekea Durban, Afrika Kusini ambako Mashindano hayo yatafanyika. Huku wakiwaomba watanzania wawaombee.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *