Hivyo ndivyo unavyoweza kuwaambia klabu ya Yanga Princess Mara baada ya kupoteza Mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake uliopigwa hapo jana katika uwanja wa Jamhuri Dodoma dhidi ya Fountain Gate Princess. Mchezo ulitamatika kwa klabu ya Yanga Princess kupoteza bao Moja kwa Sifuri.

Mchezo ule ulikuwa wa kisasi Mara baada ya klabu ya Yanga kupoteza Mchezo katika Mzunguko wa kwanza uliopigwa pale Uwanja wa Uhuru. Kipimo kilekile walichokipata jana ndicho walichokipata kwenye Mchezo wa kwanza ambao nao walikufa bao moja kwa sifuri.

Kama kuna kitu kinavutia zaidi katika Mchezo huo basi ni muuaji aliyewahukumu katika Mchezo wa kwanza, alirudi tena kwenye Mchezo wa Jana na kuwahukumu tena. Cynthia Musungu aliwafunga Uwanja wa Uhuru alirudi kuwafunga tena Uwanja wa Jamhuri Dodoma. Ni kama anajisikia vizuri zaidi kuwafunga klabu ya Yanga Princess.

Baada ya mchezo huo wa Jana klabu ya Fountain Gate Princess inafikisha alama 23 huku wakiwa sawa na Simba Queens nao wenye alama 23 tofauti ni katika Mabao ya kufunga na kufungwa ambapo inawapa faida klabu ya Simba Queens kuongoza Ligi hiyo.

Kama kuna Klabu ambayo Mashabiki na Viongozi wa Klabu ya Yanga Princess wanaweza kuikumbuka sana katika msimu huu wa Ligi kuu Wanawake basi ni Fountain Gate Princess. Kwa Msimu huu imeshindikana kupata alama kwa Fountain Gate Princess, wajaribu tena Msimu ujao.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *