Afisa Mtendaji wa Fountain Gate Sports ndugu Thabithy Kandorro amekutana na mwakilishi wa La Liga kwa nchi za Tanzania, Burundi, Uganda na Rwanda ndugu Jorge Gazapo kwa mazungumzo yanayohusu maendeleo ya Mpira wa Wanawake ndani ya Fountain Gate Princess na Fountain Gate Academy na uwepo wa La Liga nchini Tanzania.

Ndugu Jorge Gazapo amefurahishwa na maendeleo makubwa yanayofanywa na Fountain Gate Sports kwa upande wa Wanawake na kuwapongeza pia kuchukua Ubingwa wa CAF African School Championships 2023 ambapo Fountain Gate wamejishindia takribani millioni mia mbili ambazo zitatumika katika kukuza na kuendeleza mpira wa Wanawake Tanzania.

Kikao hiki baina ya Taasisi hizi mbili kinaweza kufungua ushirikiano mkubwa ambao utaimarisha mahusiano na kukuza mpira wa wanawake Tanzania.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *