Ligi ya wanawake inarejea Jumatano hii ambapo Fountain Gate Princess watashuka dimbani kuchuana na wenzao Baobab Queens kutoka Dodoma.

Mechi hii itaonyesha ubabe wa timu hizi mbili ambazo zinapigania ubingwa wa Ligi ya Wanawake mwaka huu wa 2022/2023.

Wiki iliyopita Fountain Gate Princess iliwafunga Alliance Girls kutoka Mwanza mabao manne kwa sufuri, mechi iliyochezwa uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Kwengineko, Baobab waliambulia kichapo cha nyumbani cha magoli mawili kwa moja kutoka kwa ‘Wananchi’ Yanga Princess.

Mechi zingine zilizoratibiwa kuchezwa wiki hii ni pamoja na:

  1. Alliance Girls vs Mkwawa Queens
  2. Fountain Gate Princess vs Baobab Queens
  3. JKT vs The Tigers Queens
  4. Ceasiaa Queens vs Yanga Princess
  5. Amani Queens vs Simba Queens

Kwengineko katika ligi ya wanaume ya chamionship, Timu ya Fountain Gate FC inasafiri kwenda Mkoani Mara kukabiliana na Biashara United tarehe 21/01/2023.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *