Thabit Kandoro amejiunga na Fountain Gate Academy Tanzania kama Mtendaji Mkuu wa masuala yote ya Michezo katika Taasisi.

Awali, Bw. Kandoro amekua Mkurugenzi wa Mashindano katika Timu za Yanga na kuiwezesha Timu kutwaa makombee yote ya ndani kwa msimu wa 2021/2022 pamoja na Timu za vijana wa wanawake kufikika hatua mbalimbali katika ligi.

Utambulisho wa Kandoro kujiunga na Fountain Gate Academy unaenda kuongeza chachu ya maendeleo na ukuaji wa Taasisi hiyo kulingana na kasi ya ukuaji wa Soka Nchini Tanzania.

Kwengineko, aliyekua Msimamizi wa masuala ya Michezo Bwana Alex Alumirah ameteuliwa kua Meneja wa Ukuaji wa Soka ya Wanawake katika Taasisi na pia kusimamia Timu ya Fountain Gate Princess na Timu itakayo shiriki mashindano ya CECAFA, GETS.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *