Kituo cha Fountain Gate Sports academy kimeanza rasmi majaribio yao ya kutafuta vijana watakao wasajili katika timu zao za U20 pamoja na inayo shiriki katika ligi daraja la kwanza, Championship.
Majaribio hayo yalianza tarehe sita na yatafika tamati tarehe saba mwezi huu wa Sita katika uwanja wa Shabiby, Gairo.
Wachezaji wote watajiunga na kambi za timu hizo mbili mapema hapo baadae.