Serengeti Lite Women Premier League inategemea kuendelea Weekend hii ambapo Kutakuwa na mchezo wa Kibabe ambapo utawakutanisha Matajiri wa Jiji la Dodoma @fountaingate_princess Dhidi ya Wekundu wa msimbazi Simba Queens kutoka Jiji la Kibiashara Dar Es Salaam.
Mchezo huo utapigwa katika Dimba la Fountain Gate Arena Mnamo siku ya Jumamosi kuanzia saa kumi kamili za jioni.
Ikumbukwe tu Ligi hiyo inaongozwa Na Simba Queens akiwa mbele kwa Alama Nne dhidi ya Anae mfuata Fountain Gate Princess mwenye Alama 44 hivyo ni mchezo mgumu na Muhimu kwa Timu zote mbili.